Mashemeji kutoana kijasho wikendi hii

Gor_Mahia_FC_(logo)

Mchuano kati ya Gor Mahia na Afc leopards almaaruf mashemeji debry uliokuwa umeratibiwa kuchezwa saa tisa jioni siku ya Jumapili kwa sasa umehairishwa na unatarajiwa kuchezwa  mwendo wa saa kumi.

Afisa mkuu mtendaji wa ligi ya KPL Jack Ogunda amesema mechi hiyo imehairishwa wakati pekee ila mikakati mengine ya mchezo huo imesalia vilevile.

Hatahivyo Ogunda amasema kuwa wameweka usalama wa kutosha katika mtanange huo ili kuepusha purukushani za hapa na pale wakati vidume hivyo vinapokutana.

Kogelo na Igwee watachuana katika uga wa kasarani Nairobi huku kila moja akijitafutia alama 3 muhimu za kusonga mbele.

Kufikia sasa afc wanashikilia nafasi ya pili kwa alama 7 huku Gor wakiwa nafasi ya 11 na alama 3