MCA wa Kwale aliekuwa ametiwa mbaroni aachiliwa

ggggggggggggggggggggggggggg

Kinara wa upinzani Raila Odinga pamoja na magavana wawili wa CORD wamefika katika makao makuu ya polisi mjini Malindi,kaunti ya Kilifi mapema leo, kulalamikia kukamatwa kwa mwakilishi wa wadi ya Kwale.

Mwakilishi huyo wa Marereni anadaiwa kutiwa mbaroni kwa madai ya kukiuka kanuni za uchaguzi mdogo wa Malindi.

Hata hivyo duru zinaarifu kuwa mwakilishi huyo tayari ameweza kuachiliwa baada ya wana-CORD kuzua vurugu katika kituo hicho cha polisi.

Haya yanajiri huku maafisa wakuu wa CORD wakikita kambi mjini Malindi kumpigia debe mgombea wao wa kisiasa Willy Mutengo kuchukua kiti cha eneo bunge hilo katika uchaguzi wa mapema juma lijalo.