Uorodheshaji wa matokeo ya mitihani huenda ukurejeshwa

Fred-Matiangi

Waziri wa elimu Fred Matiangi amesema kuwa wizara yake imeandaa kikao cha kujadili kurejeshwa kwa hafla za kutangazwa kwa matokeo ya mitihani nchini.

Matiangi amesema kuwa utangazaji wa matokeo hayo huleta ushindani mkali dhidi ya wanafunzi ,jambo linalochangia katika matokeo mazuri kwa wanafunzi nchini.

Huku hayo yakijiri bunge la kitaifa limewasilisha hoja bungeni ya kutaka kurejeshwa hafla hizo.

Hatua hii inajiri baada ya aliyekuwa waziri wa elimu nchini Jacob Kaimenyi kupiga marufuku mitihani ya kitaifa kutangazwa paruwanja na kwa mbwembwe.