Kampeni mjini Malindi na Kericho kukamilika kesho

Kampeni za kisiasa mjini Malindi na Kericho zitafika kikomo hapo kesho.
Hayo yanajiri huku viongozi mbalimbali wakionekana kuongeza juhudi zao za kutafuta uungwaji mkono saa chache tu kabla ya kampeni hizo kukamilika.
Viongozi kutoza serikalini na wale wa upinzani wamekita kambi katika maeneo hayo ili kuwashawishi wakaazi hao kuwachagua viongozi kutoka mirengo yao.
Mjini Malindi naibu rais William Ruto anaongoza utaftaji wa kura dhidi ya mgombea wa chama cha Jubilee Philip Charo akiwataka waunge mkono Jubilee ili kuona wanaingia serikalini baada ya uchaguzi mdogo.
Kwa upande mwengine viongozi wakuu wa CORD wako mjini Malindi kumpigia debe mgombea wao Willy Mutengo.
Chaguzi ndogo katika maeneo hayo zitafanyika tarehe 7 juma lijalo.