Kenya yaungana na mataifa mengine kusherehekea siku ya wanyama pori

 

Huku Kenya ikiungana na mataifa mengine duniani kusherehekea siku ya wanyamapori duniani, serikali ya Kenya imepiga hatua kubwa kwenye vita dhidi ya uwindaji haramu kufuatia sheria kali zilizowekwa dhidi ya uwindaji.

Jem Nyamu kutoka kituo cha Elephant Neighbour Centre amesema idadi ya uwindaji haramu wa ndovu imepungua huku uwindaji wa vifaru ukionekana kukithiri zaidi nchini.

Nyamu amesema kuna haja ya kulizungumzia swala la migogoro baina ya binadamu na wanyamapori kwani limesababisha kupungua kwa wanyama kwenye mbunga zao.

Siku hii aidha inatukumbusha jukumu la kusitisha uhalifu wowote unaoambatana na wanyamapori kwani linaathiri mazingira na uchumi wa taifa.

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita serikali imeweka mikakati zaidi ya kupunguza uwindaji haramu kufuatia ongezeko la visa vya kuawawa kwa ndovu pamoja na Vifaru nchini.