Wawili wafikishwa mahakamani kwa kupatikana na dawa za kulevya JKIA

Raia mmoja wa Nigeria na mwengine kutoka Ghana wamefikishwa katika mahakama ya Kibera baada ya kupatikana na dawa za kulevya aina ya Heroin katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Mkuu wa ujasusi katika viwanja vya ndege nchini Joseph Ngisa amesema wawili hao walikamatwa Jumatatu na kuzuiliwa hadi leo ili kutoa muda kwa maafisa wa upelelezi kuchunguza viwango vya mihadarati hiyo.
Ngisa amewaambia wanahabari kwamba tayari serikali imetathmini kuwa mihadarati hiyo ilikuwa ni ya kilo 4.9 huku raia wa Nigeria akibeba kilo moja ya Heroine yenye thamani ya million 17.
Wawili hao walikuwa wakisafiri kuelekea nchini kwao katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.