Serikali kuu yashtumiwa kwa kutekeleza majukumu ya serikali za kaunti

 

Serikali kuu inazidi kushtumiwa kwa kuendelea kutekeleza majukumu ambayo yamehamishwa katika serikali za kaunti.

Mkurugenzi Cornelius Oduor kutoka taasisi inayosimamia masuala ya kidemokrasia,amesema kuwa ikiwa serikali haitakoma swala hilo basi ugatuzi utakuwa hatarini.

Oduor aidha amehoji kutokuwa na uwazi baina ya serikali za kaunti na serikali kuu.

Wakati huo huo Oduor ametoa wito kwa serikali kuu,vita dhidi ya ufisadi vipewe kipau mbele katika mashirika yanayoshughulikia maswala ya vijana.