Uchunguzi kuanzishwa kufuatia ongezeko la udanganyifu katika mtihani wa KCSE

Rais Uhuru Kenyatta amewaagiza waziri wa elimu Fred Matiangi na mwenzake wa usalama wa kitaifa Joseph Nkaissery kuanzisha uchunguzi kufuatia kuongezeka kwa visa vya udanganyifu katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.
Haya ni baada ya matokeo ya zaidi ya wanafunzi elfu 5 waliokalia mtihani huo kufutiliwa mbali kufuatia madai ya udanganyifu, hii ikiwa ongezeko la asilimia 70 la kiwango cha visa vya udanyanyifu ikilinganishwa na mwaka 2014.
Huku ikizingatiwa ongezeko hilo la visa vya udanganyifu mwaka huu, Matiangi amesema kuwa hawatafutilia mbali matokeo ya shule nzima, na badala yake watatafuta mbinu kwa wanafunzi walioathirika pamoja na familia zao kupata majibu.
Ni kaunti ya Isiolo pekee kati ya kaunti zote 47, ambayo haikuwa na visa vya udanganyifu wa mitihani hiyo, huku vituo 305 vikiathirika na visa hivyo kote nchini.
Ripoti kamili kuhusu hali hiyo aidha inatarajiwa kutolewa katika muda wa mwezi mmoja.
Aidha wanafunzi zadi ya 300,000 walioshiriki mtihani huo hawakufiskisha kiwango cha alama zinazohitajika ili kijunga na vyuo vikuu ni asilimia ya 70 ya wanafunzi hao.
Ameongeza kuwa idadi kubwa ya walimu kutotekeleza majukumu yao ipasavyo pamoja na mgomo uliodumu mwezi mmoja mwaka uliopita ni maswala yaliyoathiri matokeo hayo.