Matokeo ya KCSE kutangazwa rasmi leo.

images (3)

Matokeo ya mtihani ya KCSE mwaka jana yanatarajiwa kutangazwa rasmi leo.

Matokeo hayo ya zaidi ya watahiniwa nusu milioni yatatolewa na waziri wa elimu Fred Matiangi katika jumba la mitihani jijini Nairobi.

Katika mitihani hiyo ya mwaka jana takriban wanafunzi 50, walimu, wanafunzi wa chuo kikuu pamoja na maafisa wa polisi walitiwa mbaroni huku simu 30 za rununu zikishikwa kutoka kwa wanafunzi hao, huku ikiarifiwa kuwa kaunti zote 47 zilishiriki udanganyifu katika mitihani hiyo ispokuwa kaunti ya Isiolo pekee huzu zaidi ya matokeo ya watahiniwa elfu 5 yakifutiliwa mbali.

Aidha katika matukio mengine baadhi ya wanafunzi walifaulu kupata makaratasi ya mitihani siku kadhaa kabla ya mitihani kufanyika.