Abdulswamad atoa wito kwa viongozi kuzingatia matamshi yao

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir, amewataka viongozi kuzingatia matamshi wanayoyatumia dhidi ya viongozi wenza akisema kuwa wakenya wengi wanakosa imani na baadhi ya viongozi kutokana na matamshi yao.
Akiongea na Radio Salaam, Nassir amesema kuwa viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa mfano bora kwa raia badala ya kurushiana cheche za matusi hadharani kila mara wanapotofautiana.
Matamshi ya kiongozi huyo yanajiri wakati ambapo viongozi kadhaa wanaendelea kushtumiana kwa maneno makali kuhusu sakata za ufisadi jambo linalowakera wakenya wengi.