Ligi ya EPL kuendelea wikendi

Ligi kuu ya premia nchini Uingereza EPL inaendelea wikendi hii ambapo mechi 6 zitachezwa kesho Jumamosi kisha mbili zisakatwe Jumapili.
Viongozi Leicester City watawakaribisha Norwich City,Chelsea watamtembelea Southmpton,West Ham United watachuana na Sunderland.
Wattford wataikabili Bournemouth,Stock City awe mwenyeji wa Aston Villa kisha West Bromwich akamilishe udhia kesho kwa kupambana na Crystal Palace.
Mechi kubwa wikendi hii itakuwa Jumapili ambapo Manchester United atachuana na Arsenal ugani Old Trafford kisha baadaye Tottenham Hotspur atachuana na Swansey City.
Liverpool na Manchester City watachuana katika fainali kuwania taji la Capital One siku ya jumapili ugani Wembley.