Nani atakaeteuliwa kuwa Rais mpya wa FIFA?

Uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA unaandaliwa hii leo katika makao makuu ya FIFA yalioko jijini Zurich nchini Uswizi.
Wagombea watano wameidhinishwa kugombea nafasi ya kumrithi Sepp Blatter aliyepigwa marufuku kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka sita.
Tokyo Sexwale wa Afrika Kusini,Prince Ali wa Jordan,Sheick Salman wa Bahrain,Jerome Champagne wa Ufaransa na Giann Infantino wa Uswizi wanashindania kiti hicho.
Tayari Ali na Jerome wameshindwa kusimamisha uchaguzi huo kuandaliwa baada ya mahakama ya michezo kukosa ushahidi kukubaliana na ombi lao.
Rais wa shirikisho la soka nchini FKF Nick Mwendwa ni miongoni mwa marais wa mashirikisho 209 wanachama wa FIFA atakayepiga kura katika uchaguzi huo.
Lazima mgombea apate zaidi ya kura 138 ili kutangazwa mshindi.