Uchaguzi wa FIFA kufanyika kesho

Marais wa mashirikisho ya soka kutoka mataifa mbali mbali ulimwenguni wanakutana jijini Zurich nchini Uswizi ambapo watamchagua rais ya shirikisho la soka dunia FIFA ijumaa hii.
Mmoja wa wagombea watano ambao wameidhinishwa kushiriki uchaguzi huo atarithi nafasi ilioachwa wazi na Sepp Blatter anayetumikia marufuku ya miaka 6 kutojihusisha na masuala ya soka.
Tunaangazia orodha ya wagombea hawa katika historia ya miaka 111 ya FIFA.
SHEIKH SALMAN BIN IBRAHIM AL-KHALIFA KUTOKA BAHRAIN
Sheikh Bin Ibarahim Al khalifa ndiye rais wa shirikisho la soka barani Asia.
Salman alikuwa anampigia debe Michael Platini katika uchaguzi wa shirikisho la FIFA mwaka jana lakini sasa ndiye mgombea anayependwa na kuenziwa na wengi baada ya Platini kufungiwa njea kwa madai ya ufisadi.
Salman akiwa na umri wa miaka 50 ameonyesha azma ya kuMrithi Blatter JAPO hajaendesha kampeni zozote lakini amefanya majadiliano mbali mabli.
Wengi wa mashabiki wa Salman wanatoka bara za Asia na Africa yalio na mataifa 100 kati ya 209 yalio wanachama wa FIFA.
GIANNI INFANTINO KUTOKA ITALIA JAPO NI MZALIWA WA USWIZI.
Akiwa amezaliwa miaka 45 iliopita karibu na rais wa zamani wa Fifa Sepp Blatter ameahidi kuongeza timu zinazoshiriki kombe la dunia kutoka 32 hadi 40 jambo ambalo lingepelekea mataifa mengi kumuunga mkono.
Infantano ambaye ni katibu wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA anajulikana kwa kuwahi kuhudumu kama rais wa shirikisho la soka barani Ulaya na amekuwa akitembea kote ulimwenguni kujipigia debe.
Anategemea pakubwa uungwaji mkono kutoka mataifa ya bara Ulaya na Amerika Kusini kwa asilimia kubwa hizi zikiwa ni kura 69 kati ya 209 zitakazopigwa.
PRINCE ALI BIN HUSSEIN KUTOKA JORDAN.
Ali ndiye rais wa shirikisho la soka nchini Jordan.
Alimpinga Sepp Blatter katika uchaguzi wa mwezi Mei mwaka jana na kumaliza nafasi ya pili.
Ali mwenye umri wa miaka 40 amekuwa akicheza siasa akitegemea pakubwa vyombo vya habari kuendesha kampeni zake na miradi mbali mbali ya soka.
Mapema mwaka huu,alilalamika kuhusu ushirikiano wa shirikisho la Afrika CAF kutangaza kumuunga mkono mpinzani wake Sheick Salman japo CAF ilikana madai hayo.
Pia Ali amewahi kuhudumu kama naibu wa rais katika shirikisho la FIFA na anawania urais kupitia sera tofauti za kuimarisha shirikisho hilo.
Ali anategemea uungwaji mkono kutoka bara Asia japo mataifa mengine kutoka bara Ulaya yameonyesha nia ya kumchagua pia.
JEROME CHAMPAGNE KUTOKA UFARANSA.
Jerome amewahi kuhudumu kama katibu mkuu wa shirikisho la FIFA kwa masuala ya kigeni.
Champagne alionyesha azma za kuwania kiti hicho lakini hakuweza kutimiza matwaka yaliyotakikana japo sasa ametimiza matawaka hayo na anatarajiwa kupambana na wenzake.
Akiwa amezaliwa miaka 57 iliopita,Jerome ameendesha za kujisimamia bila msaada kutoka mashirika yoyote licha ya wagombea wenza kushuku fedha hizo na kutaka achunguzwe.
Haieleweki jinsi atakavyopata uungwaji mkono kwani hakuna shirikisho au bara ambalo limetangaza nia ya kumchagua katika uchaguzi huo.
TOKYO SEXWALE KUTOKA AFRIKA KUSINI.
Sexwale ambaye ameonyesha umarufu wake kwa kutaka kushinda kiti hicho amewewahi kuwa mfungwa katika gereza la Robben Island wakati wa enzi wa marehemu Nelson Mandela.
Akiwa amezaliwa miaka 62 iliopita,umarufu wake umekuwa kwa kiasi kikubwa kupitia lengo lake la kutaka kutatua tofauti zilizopo dhidi viongozi wa soka katika ya nchi ya Israel na Palestine .
Lakini kampeni zake zimekuwa kikikumbwa na uhasama baina ya viongozi wengine wakimwambia kuwa licha ya kuwa na urafiki na rais wa zamani wa Afrika Kusini sio sababu kuu ya yeye kutaka kuwania kiti hicho na haihusiani vyovyote na soka.
KUHUSU UCHAGUZI
Na ikiwa tumeangalia viongozi hao tofauti,marais wa mataifa 209 ndio watakua na uamzi wa mwisho.
Hata hivyo,haijulikani iwapo mataifa ya Kuwait na Indonesia yataruhusiwa kushiriki uchaguzi huo baada ya serikali za mataifa hayo kukashiiwa na FIFA kwa kuingilia masuala ya soka na iwapo yatapigwa marufuku basi ni mataifa 207 yatapiga kura.
Lazima mshindi apate kura zaidi ya 138 na ikiwa hatafikisha,atahitajika kupata kura 104 katika raundi ya pili na katika kila raundi mgombea wa mwisho anatimuliwa ili kubakisha wengine kuwania nafasi hiyo.
Shirikisho la FIFA lilibuniwa mwaka wa 1904 na halikuwahi kuandaa uchaguzi hadi kufikia 1961 ambapo walimchagua Stanley Rous na kufuatiwa na Joho Havelange katika mwaka wa 1974 .
Havelenge raia wa Brazil aliongoza FIFA kwa miaka 24 kabla ya Blatter kuchukua uongozi huo.