Kijana shabiki wa Messi aliyevaa jezi ya mfuko wa plastiki apata jezi kutoka kwa Messi

Kijana wa taifa la Afghanistan alievaa fulana ya mfuko wa plastiki ilio na jina la nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amepata jezi kutoka kwa mshambulizi huyo.
Baada ya kumtafuta mtoto huyo ambaye ni shabiki mkubwa wa Messi raia wa Argentina,amempata na kumkabidhi jezi hiyo.
Murtaza Ahmadi mwenye umri wa miaka 5 amepatikana katika wilaya ya Jaghori mashariki mwa mkoa wa Ghazni nchini Afghanistan.
Murtaza alitumiwa jezi ya Mess iliotiwa saini pamoja na mpira kutoka kwa mshambuliazi huyo wa Barcelona ambaye ametuzwa kuwa mchezaji bora mara tano.
Msako wa mtoto huyo katika mtandao ulisababishwa na picha moja ilioenea katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha amevaa fulana ya plastiki ya Messi.