Hatimaye Messi amfunga Cech

LONDON, ENGLAND - AUGUST 24: Petr Cech of Arsenal looks on during the Barclays Premier League match between Arsenal and Liverpool at the Emirates Stadium on August 24, 2015 in London, United Kingdom. (Photo by Julian Finney/Getty Images)
Lionel Messi amefanikiwa kumfunga kipa Petr Cech baada ya kusubiri kwa zaidi ya saa 10 na dakika 11.
Messi alifunga mabao 2 kuisaidia Barcelona kuitandika Arsenal mabao 2-0 katika mechi ya kuwania taji la klabu bingwa ugani Emirates nchini Uingereza.
Ilikua ni mechi yake ya saba dhidi ya Petr Cech na sasa anafikisha idadi ya mabao manane ambayo amewafunga Arsenal kufikia sasa. Barcelona wametumia mechi hiyo kuweka rekodi yao ya kucheza mechi 33 bila kupoteza mechi yeyote.
Muajentina huyo sasa amefunga mabao 51 katika mechi tofauti za klabu bingwa japo Raul na Chrstiano Ronaldo wanaongoza kwa mabao 56 na 60 mtawalia. Katika matokeo mengine Juventas ikicheza nyumbani imelazimisha sare ya mabao 2-2 na Beryan Munich.
Mechi hizo zinaendelea leo ambapo Dynamo Kiev itaikaribisha Manchester City huko Ukraine na PSV Eindhoven kutoka Uholanzi wawalike Atletico Madrid.