Wakaazi wa Lamu kujiandikisha kura baada ya uchaguzi wa Malindi

Wananchi wa kaunti ya Lamu wataanza kujiandikisha kama wapiga kura baada ya uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi tarehe 7 mwezi ujao.
Mshirikishi wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kanda ya Pwani Kaskazini,Amina Sudi amesema kesi iliyokuwa mahakamani baina ya gavana Issah Timammy na aliyekuwa mpinzani wake Fahim Twaha ilisababisha kuchelewesha zoezi hilo.
Aidha,Amina amesema kuwa zoezi hilo pia litaendeshwa katika eneo bunge la Malindi pindi tu baada ya uchaguzi mdogo kuandaliwa na litatengewa muda wa mwezi mmoja kama maeneo mengine.
Zoezi la uandikishaji wa wapiga kura limekua likiendelea kwa wiki mbili sasa ambapo Amina amewataka wananchi wa sehemu hizo kujitokeza kwa wingi watakapoanza kuwaandikisha.