Walimu wanaoadhibu wanafunzi kuchukuliwa hatua kali

Waziri wa elimu nchini,Fred Matiangi ameamuru kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa walimu wanaowachapa wanafunzi katika kaunti ya vihiga.
Matiangi ameyasema haya akiwa katika ziara yake katika shule ya wasichana ya Keveye iliyoko katika kaunti hiyo ya Vihiga.
Waziri huyo ameongezea kuwa anatarajia ripoti kuhusu walimu hao siku ya Jumatatu na iwapo watapatikana na hatia basi wataadhibiwa kulingana na sheria.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya video kuibuka katika mtandao wa kijamii wa Facebook ilionyesha walimu wa shule hiyo wakiwachapa na kuwaadhibu wananfunzi.