Duale akana kuhusika na sakata ya NYS

Kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Daule amepinga vikali madai kwamba alihusika katika sakata ya NYS ya shilingi milioni 791.
Duale akijibu taarifa ya Waiguru hapo jana,amepinga vikali kuhusishwa na sakata hiyo na kuapa atapambana na Waiguru iwapo hatotoa ushahidi.
Aidha Duale amemtaka Waiguru kukoma kuwachafulia viongozi na wafanyikazi wa serikali jina ilhali wizi huo wa shilingi milioni 791 ulimhusu yeye na jamaa zake.
Wakati huo huo naye mbunge wa Nandi Hills Alfred Keter amewametaka kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale ,Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na msaidizi wa naibu rais Farouk Kibet kujiuzulu kwenye wadhifa wao ili kupisha uchunguzi wao.