Kenya yatia sahihi mkataba na Israel

NETD

Rais Uhuru Kenyatta amesaini mkataba na serikali ya Israel kufadhili miradi kadhaa humu nchini ikiwemo usalama,kilimo na maji.

Rais ambaye yuko nchini Isreal kwa ziara ya siku 3 amekutana na mwenyeji wake Benjamin Netanyahu ambapo wamekubaliana kushirikiana kupiga vita ugaidi ambao wameutaja umeathiri mataifa mengi ulimwenguni.

Rais ameipongeza Israel kwa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono mradi wa kilimo wa Galana Kulalu ambao amesema utakapotekelezwa utamaliza ukosefu wa chakula nchini.

Naye Netanyau amesema Israel imekua na uhusiano wa karibu na Kenya na kwamba itaimarisha ushirikiano huo zaidi kuhakikisha wananchi wa mataifa hayo wanapata maendeleo.

Katika ziara yake,rais Uhuru Kenyatta amepanda mti wa zeituni katika shamba maalum ambalo marais wageni huzuru nchini Israel.