EACC yamchunguza upya Nzibo

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC inamchunguza upya afisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Yusuf Nzibo kwa tuhuma za ufisadi kwenye sakata ya ununuzi wa vifaa 20 vilivyotumika kwenye uchaguzi mkuu uliopita almaarufu Chicken Gate.
Kwa mujibu wa tume hiyo wamepata ushahidi kutoka mataifa ya kigeni kuhusu kamishna huyo na hivyo basi kumfungulia mashtaka upya huku tume hiyo ikimhoji Nzibo kwa zaidi ya masaa mawili.
Maafisa wa tume hiyo wamesema kuwa wanatarajia kukamilisha uchunguzi huo na kumkabidhi mapendekezo yao kiongozi wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko ili kuwachukulia hatua za kisheria wahusika.