Waititu aunga mkono kuundwa kwa jopo maalum kumchunguza Tonui

Mbunge wa Kabete Ferdinand Waitutu ameunga mkono hatua ya rais Uhuru Kenyatta kuunda jopo litakalo mchunguzi jaji Philip Tonui aneyakabiliwa na madai ya ulaji rushwa.
Hata hivyo Waititu amesema licha ya yeye kutaka ukweli ufahamike na haki ipatikane katika kesi hiyo ila hatowania kiti cha ugavana wa kaunti ya Nairobi ifikapo mwaka 2017.
Aidha mbunge huyo amedokeza kuwa muungano wa jubilee unaweka mikakati yakuhakikisha kuwa chama cha jubilee kina shinda kiti hicho cha ugavana wa Nairobi ifikiapo mwaka ujao.