Kongamano la Umoja wa Afrika la maji laingia siku ya pili

Kongamano la Umoja wa Afrika la maji katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi limeingia siku yake ya pili hii leo.
Kongamano hilo la wiki moja na ambalo linaandaliwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza linawaleta pamoja viongozi mbalimbali wa sekta ya maji kutoka bara Afrika na mataifa mengine ulimwenguni,kujadili mbinu bora za kutoa huduma za maji safi kwa wananchi.
Waziri wa maji Eugine Wamalwa amesema Kenya itatumia kongamano hilo kutafuta ushirikiano kutoka mataifa yalioendelea ili kumaliza changamoto ya wananchi kukosa maji safi katika maeneo yao.