Mechi baina ya Dortmund na Leverkusen yasimamishwa baada ya refa kuondoka uwanjani

jj

Refarii mmoja nchini Ujerumani ameshangaza mashabiki wa soka baada yake kuondoka uwanjani na kuacha mechi imesimama.

Felix Zwayer aliondoka baada ya meneja wa Bayer Leverkusen Roger Schmidt kukataa kutii amri yake ya kumfurusha uwanjani kwa kosa la kulalamika sana.

Mechi hiyo ya ligi ya Bundesliga baina ya Borussia Dortmund na Leverkusen ilicheleweshwa kwa dakika 8 ambapo mwishowe Schmidt alikubali kuondoka eneo la kiufundi.

Schmidt amedai bao hilo lililofungwa na Pierre-Emerick Aubameyang halikufaa kukubaliwa kwani mkwaju wa adhabu uliosababisha bao haukupigiwa eneo sahihi.

Refa huyo alimsihi nahodha wa Leverkusen Stefan Kiessling aliyefanya madhambi yaliyosababisha mkwaju huo wa adhabu amsihi meneja wake aondoke bila ufanisi.

Baada ya hilo kushindikana Zwayer aliondoka uwanjani na kuingia chumba cha kubadilishia mavazi ambapo alifuatwa na wachezaji baadaye.