Suarez asahau paspoti nyumbani

Luis-Suárez-Uruguay-Liverpool-Barcelona

Arsenal inaomboleza baada ya kubaini kwamba Luis Suarez amepata paspoti yake aliyokua amesahau alipokua anapanga kusafiri kuelekea Uingereza.

Suarez aliwashangaza wengi baada ya kusema amesahau pasipoti yake nyumbani kabla ya Barcelona kuondoka kuelekea jijini London.

Ilibidi mmoja wa maafisa wa Barcelona kuagizwa kurudi hadi kwa nyumba ya ya raia huyo wa Uruguay ili kuichukua mda mfupi kabla ya kuondoka na kikosi kizima cha Barcelona.

Amefanya katika uwanja wa Emirates mapema leo na kuwaacha mashabiki wa The Gunners kuomba tu achanganyikiwe asije akawaangimiza vijana wao wanapokutana jioni hii.

Suarez na wauaji wenzake Lionel Messi na Neymar wamefunga mabao 91 kati yao msimu huu huku Suarez akifunga mabao 41.

Mechi hiyo itachezwa ugani Emirates kuanzia 10:45 usiku wa leo.