Trabzonspor atimuliwa uwanjani kwa kumuonyesha refa kadi nyekundu

Mchezaji wa klabu ya Trabzonspor ya Uturuki Salih Dursun ametimuliwa uwanjani baada ya kumuonyesha refarii kadi nyekundu.
Ilikua dakika ya 86 ambapo refa Denis Bitnel alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja mchezaji Luis Cavanda kwa kucheza visivyo ndani ya eneo la hatari.
Hapa wachezaji wa Trabzospor walimzingira refa kupinga kadi hiyo ambapo, Dursun walimzingira refa kupinga kadi hiyo na kumuonyesha pia hatua iliopelekea na yeye kufukuzwa uwanjani.
Tukio hilo limetokea katika mechi ambayo Trabzonspor wametandikwa mabao 2-1 na Galatasaray katika mechi ya Ligi Kuu ya Uturuki ambapo wamelazimika kusalia na wachezaji 9 uwanjani.
Sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kujipata pabaya na marefa.
Mwezi Novemba mwaka jana,mwenyekiti wa Trabzonspor Ibrahim Haciosmanoglu alipigwa marufuku ya siku 280 baada ya kuwafungia marefa wanne uwanjani kwa kushindwa kutoa penati kwa klabu yake