Manchester United yafuzu katika robo fainali ya michuano ya FA

39387

Manchester United itakutana na West Ham United katika hatua ya robo fainali kuwania taji la FA nchini Uingereza msimu wa mwaka 2015/2016.

United ilifuzu robo fainali baada ya kuitandika Shrewsbury Town mabao 3-0 hapo jana usiku.

Mabao ya United yamefungwa na wachezaji Chris Smalling ,Juan Mata na Jesse Lingard.

Katika mechi zingine,Chelsea itamenyana na Everton,Crystal Palace waikabili Reading ,Watford watachuana na mshindi baina ya Arsenal au Hull City mtawalia.

Mechi za robo fainali zitachezwa wikendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.