Rubani mkorofi ahojiwa Kileleshwa

Rubani wa ndege ambaye alinaswa na video akimdhalilisha afisa mmoja wa polisi katika kaunti ya Nyandarua anaendelea kuhojiwa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kileleshwa.
Duru zimearifu kuwa rubani huyo amefika katika kituo hicho baada ya shinikizo za wakenya kupitia mitandao ya kijamii kushinikiza kukamatwa kwake.
Hapo awali Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet aliamuru kukamatwa na kufunguliwa mashtaka mara moja kwa rubani huyo.
Boinet amesema kuwa rubani huyo kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kama njia moja wapo ya uchunguzi dhidi ya tukio hilo ambalo limezua hisia mseto miongoni mwa wakenya katika mitandao ya kijamii.