Wanaoogelea sehemu hatari kuchukuliwa hatua kali Kilifi

watamu-beach-pano-dec-2013

Polisi katika kaunti ya Kilifi wamewaonya wananchi wanaoogelea maeneo hatari baharini kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa kiuka onyo hilo.

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Alexandar Makau amesema wameafikia hatua hiyo baada ya mwanafuunzi wa chuo kikuu cha Pwani kufa maji alipokua akiogelea katika fuo za Baobab jijini Kilifi.

Shem Mochache alikufa maji alipokua akiogelea na wenzake ambapo kwa sasa mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali kuu ya Kilifi.

Aidha Makau amesema kuwa idara ya usalama itafanya kampeni za uhamasisho ili kuwapa wageni na wanafunzi ufahamu zaidi kuhusiana na fuo za mji huo ili kuepuka maafa zaidi.