Uhuru amsimamisha kazi Tunoi na kuunda jopo maalum

images (7)

Rais Uhuru Kenyatta amemsimamisha kazi jaji wa mahakama ya juu zaidi Philip Tunoi na kuunda jopo litakalochunguza madai ya ufisadi dhidi ya jaji huyo.

Jopo hilo maalum la watu saba litakaloongozwa na Rashad Rao ili kuchunguza madai hayo ikiwemo utendakazi wake pamoja na kosa la kukubali hongo ya shilingi milioni 200 pamoja na kukiuka utaratibu wa idara ya mahakama.

Jopo hilo linahusisha jaji Roselyn Korir,jaji mstaafu Jonathan Havelock,Judith Guserwa,James Kaberere Gachoka,Abdirashid Abdullahi Hussein na George Munji Wakukha.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya mawakili kusema kuwa huenda rais Uhuru Kenyatta akaondolewa mamlakani kwa kukiuka katiba akiwa angedinda kuteuwa jopo hilo kufikia leo.

Jaji Tunoi anakabiliwa na kosa la kukubali hongo ya shilingi milioni 200 kutoka kwa gavana wa kaunti ya Nairobi Evans Kidero ili kumpendelea katika kesi ya kupinga uchaguzi wake mwaka 2013.