Senate yapendekeza bajeti ya usalama kutengewa NPSC badala ya wizara

Kamati ya Usalama katika bunge la Senate imependekeza bajeti inayotengewa idara ya polisi kupewa tume ya huduma za polisi chini ya Jonstone Kavuludi kuanzia mwaka huu badala ya kutolewa kupitia wizara ya usalama wa ndani.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Yusuf Haji katika kikao cha kutathmini bajeti ya idara hiyo amesema pendekezo lao lingesaidia kuondoa ubadhirifu na kuhakikisha pesa hizo zinatumika kwa shughuli zinazotengewa.
Aidha Kamati hiyo inashinikiza wizara ya fedha kupiga marufuku ukodishaji wa magari ya polisi na kutenga pesa kwa ununuzi wa magari zaidi, hali ambayo kamati inasema imetatiza utendakazi wa polisi na kuhatarisha maisha yao.