Washukiwa 5 wa wizi wauwawa Nairobi

Washukiwa watano wa wizi wameuwawa katika tukio la kufyatuliana risasi baina yao na maafisa wa polisi katika barabara kuu ya Thika jijini Nairobi.
Kulingana na maafisa hao ni kuwa wamewauwa wezi hao katika eneo la chuo kikuu cha KCA mkababala na shirika la huduma kwa vijana NYS na kupata bunduki aina ya AK47,bastola mbili pamoja na gari yao.
Maafisa wa polisi wameongeza kuwa kundi hilo lilijaribu kutekeleza uhalifu katika eneo la Hurlingham viungani mwa jiji lakini wakafanikiwa kukwepa mtego wa polisi waliokuwa wakishika doria.