Ayiemba kutaja kikosi kitakachoshiriki michuano ya IRB Sevens

Kocha wa timu ya taifa ya raga wachezaji saba upande Benjamin Ayiemba atataja kikosi kitakachoshiriki michuano ya dunia ya msururu wa IRB Sevens Series hapo kesho.
Makala yajayo yataandaliwa jijini Las Vegas tarehe 4-6 mwezi ujao kisha Vancouver tarehe 12-13 mwezi ujao.
Ayiemba atataja kikosi hicho katika uwanja wa RFUEA jijini Nairobi ambapo ataelezea mipango alio nayo kuimarisha matokeo zaidi ya alioyaandikisha katika makala ya Wellington na Sydney.
Kenya imejumuishwa kundi ‘A’ pamoja na New Zealand,Ureno na Urusi. Shujaa kwa sasa inashikilia nafasi ya 8 katika jedwali la dunia kwa alama 42. Vijana hao wataondoka nchini tarehe 28 mwezi huu kuelekea Las Vegas.