Wamiliki wa leseni za silaha kujisajili upya

download

Waziri wa maswala ya ndani nchini Joseph Nkasseiry ametoa makataa ya siku 30 kwa raia wote wenye leseni za kumiliki silaha kuzisajili upya.

Kwa mujibu wa Nkaissery asilimia kubwa ya wanaomiliki silaha hizo wanatumia leseni bandia baada ya kuwahonga maafisa wa polisi.

Haya yamejiri sikuu chache tu huku baadhi ya raia wakilalamikia watu ambao wamekuwa wakitumia silaha zao vibaya kwa kujeruhi na kuua bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.