Waiguru ahojiwa na EACC baadab ya kuzuka madai mapya

Aliyekuwa waziri wa ugatuzi Ann Waiguru amehojiwa katika tume ya kukabiliana na ufisadi nchini EACC kuhusu sakata inayokumba shirika la huduma kwa vijana NYS.
EACC ilihitaji maelezo muhimu kutoka kwa Waiguru baada ya madai mapya kuibuliwa na Josphene Kabura kwamba alimtumia katika ubadhirifu wa shilingi milioni 791 za NYS kupitia kandarasi gushi.
Nae Josephene Kabura anatarajiwa kufika mbele ya tume hiyo hapo kesho kuelezea anachokifahamu kutokana na stakabadhi alizosaini akidai Waiguru alihusika katika sakata hiyo.
EACC kwa upande wake imekana madai kwamba ilimwondolea Waiguru makosa yote kuhusu sakata hiyo wakati ilipotangaza kwamba amepatikana bila hatia wiki mbili zilizopita na kwamba uchunguzi kumhusu unaendelea.