Wito watolewa kwa wananchi kupiga ripoti endapo watapata habari za simba mtaani licha ya matumaini kuwa wamerudi mbugani

images (4)

Maafisa wa shirika la huduma kwa wanyama pori nchini KWS wameamka kwa kuendeleza kuimarisha doria,katika mbuga ya wanyama ya Nairobi ili kuhakikisha kwamba simba sita waliotoroka wamethibitishwa kurudi mbugani.

Kwa mujibu wa mkurugenzi anayehusika na usimamizi wa wanyama hao kati mbuga hiyo Patrick Omondi,ni kuwa maafisa wake wameimarisha doria katika msitu ulioko karibu na kambi ya wanjeshi ya Langata.

Licha ya Omondi kuwa na matumaini kwamba simba wote walirejea nyumbani,amewataka wananchi kupiga ripoti kwao endapo watamuona ama kupata habari za simba yeyote mtaani.