Viongozi wa CORD kuwatimua wanaoasi chama hicho

Viongozi kutoka muungano wa CORD wamesema hawatasita kuwatimua chamani viongozi wote ambao wameasi vyama vya muungano huo kwa kujiunga na upande wa serikali.
Kulingana na mbunge wa Westlands Timothy Wanyonyi ni kuwa kwa mazingatio ya sheria ya vyama vya kisiasa,ni marufuku kwa viongozi kuwafanyia kampeni vyama pinzani.
Baadhi ya wabunge kutoka kaunti ya Kilifi wamekuwa wakitajwa kuwa miongoni mwa watakaotimuliwa chamani.