Seneta wa Kwale aanzisha kampeni ya kuhamasisha wapwani kujiandikisha kama wapiga kura

mmmm

Seneta wa kaunti ya Kwale Boy Juma Boy amesema wameanzisha kampeni ya kuhamasisha wakaazi katika kanda ya Pwani kujiandikisha kwa wingi kama wapiga kura ili kuwachagua viongozi bora na sio bora viongozi.

Boy amesema hatua ya idadi kubwa ya wapwani kuwa na historia ya kutojiandikisha kwa wingi kama wapiga kura, ilisababishwa na kampeni iliyokuwa ikiendeshwa awali kwa lengo la kufaidi baadhi ya viongozi.

Kiongozi huyo amesema endapo wapwani watajiandikisha kwa wingi safari hii, hakuna shaka changamoto zinazokumba kanda hiyo zitapata suluhu la kudumu.