EACC yasema ilimuondolea Waiguru lawama kwa maswala mengine ila sio sakata ya milioni 791

Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi EACC imesema kuwa ilimuondolewa lawama aliyekuwa waziri wa Ugatuzi Anne Waiguru kwa maswala mengine lakini siyo sakata ya NYS ya shilingi milioni 791.
Katika kikao na waandishi wa habari mwenyekiti wa tume hiyo Philip Kinusu amesema kuwa uchunguzzi kuhusu sakata ya NYS ulitekelezwa na kitengo cha ujasusi bila ya kuhusisha tume hiyo.
Ameongeza kuwa tume hiyo iliamua kuanzisha upya uchunguzi dhidi ya Waiguru baada ya mfanyibiashara Kabura Irungu kuibua madai mapya kuhusu sakata hiyo
Kinusu ameahidi kuendeleza uchunguzi huo na kisha kutoa mapendekezo kwa afisi ya mkurugenzi wa upelelezi nchini.