Baadhi ya wawakilishi wa wadi Taita Taveta wataka hatua kuchukuliwa dhidi usafirishaji wa wapiga kura

images (8)

Zoezi la usajili wa wapiga kura likiendelea kote nchini,baadhi ya wawakilishi wa wadi katika kaunti ya Taita Taveta wametaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya wanasiasa wanaosafirisha wapiga kura kutoka kaunti nyengine hadi katika kaunti hiyo.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha ODM katika eneo bunge la Voi John Manyama viongozi hao wameitaka tume ya uchaguzi kuelezea wazi iwapo ni sawa kwa wapiga kura kutoka kaunti zengine kusafirishwa na wanasiasa na kujiandikisha kama wapiga kura huku akisema kuwa huo ni ufisadi mkubwa wa siasa.

Hata hivyo Manyama amewataka wananchi wa kaunti hiyo kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ili kuwachagua viongozi waadilifu.