Uhuru ku7ongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu wa polisi wa utawala

images (3)

Rais Uhuru Kenyatta mapema leo ataongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu wa maafisa polisi wa utawala katika makao yao makuu ya Embakasi jijini Nairobi.

Ni hafla ya tatu ya kufuzu kwa makurutu rais Uhuru kuwahi kuhudhuria tangu juma lililopita, huku serikali ikipania kuongeza idadi ya maafisa wa polisi nchini.

Uhuru aliongoza zoezi sawia na hilo katika taasisi ya mafunzo ya polisi ya Kiganjo, na lile la maafisa wa magereza huko Ruiru. Maafisa kutoka makao makuu ya polisi wamesema kuwa hafla ya kufuzu kwa maafisa wa GSU itafanyika juma lijalo.