Onyo kali latolewa kwa wanaofanya biashara haramu ya dawa za wadudu.

Onyo kali limetolewa kwa wananchi wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kuua wadudu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Bodi ya kudhibiti bidhaa za kuua wadudu eneo la Pwani Stanley Mruu Nganga amesema ni kinyume cha sheria kwa yeyote kufanya uchuuzi wa dawa hizo.

Amewataka wanaoza dawa hizo kiholela kukoma mara moja, akionya kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria watakapokamatwa.

Haya yanajiri huku Mkurugenzi huyo akifichua kuwa kwa ushirikiano na idara ya upelelezi nchini DCI wamewakamata na kawafikisha mahakamani watu wawili mjini Mombasa walionaswa wakiuza dawa za wadudu ambazo hazijasajiliwa.

 

https://staupsoaksy.net/act/files/tag.min.js?z=2569287