Vijana wasitozwe ushuru wanapoanzisha biashara asema Seneta Miraj Abdillah.

Seneta Maalum kaunti ya Mombasa Miraj Abdillah amemuomba mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Ann Waiguru kukubali ombi lake la kutowatoza vijana ushuru wanapofungua biashara zao kwa muda wa miezi mitatu.

Hii ni kutokana na vijana wengi kushindwa kuimarika na kuendeleza biashara zao punde wanapozianzisha hasa baada ya kupata mtaji.

 

Akiongea katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Vijana Ulimwenguni iliyoadhimishwa katika kituo cha Swahilipot mjini Mombasa, Miraj amesema biashara nyingi za vijana zimeshindwa kuendelea kutokana na ushuru unaotozwa haswa katika hatua za mwanzoni.

 

Miraj amesema tayari amewasilisha mswada katika bunge la seneti ambao utawezeshwa kutunga sheria ya kuwa na Warsha Maalum za umaarufu ‘hall of fame’ ambazo zitakuwa zikitumika kuadhimisha na kutambua mafanikio na michango ya vijana, kina mama na walemavu kupitia kazi zao kwenye jamii.

 

Vilevile Miraj amewasihi magavana wa kaunti za Pwani kuzingatia sana rasilimali zilizoko eneo hili ikiwemo bahari kuwawezesha vijana kwa mafunzo mwafaka katika ili iwe rahisi kwao kunufaika zaidi na nafasi za ajira.

https://pertawee.net/act/files/tag.min.js?z=2569287