Ahueni 318 wakipona wakati Taifa likikosa kurekodi Kifo Chochote
Jumla ya watu 114 wameripotiwa kuambukizwa virusi vya korona katikakipindi cha saa 24 zilizopita na kufikisha idadi ya jumla ya maambukizi 34, 315 kuanzia kuripotiwa kwa kisa cha kwanza mnamo Machi 13 mwaka 2020.
Kulingana na Aman watu kati ya kesi zote zilizoripotiwa hii leo mmoja pekee alikuwa raia wa kigeni huku 93 wakiwa wanaume na 21 wakitokea jamii ya kike .
Aidha Kaunti ya Mombasa imeongoza kwa kurekodi visa 17 ikifuatiwa na kaunti ya Nairobi na visa 16. Maeneo bunge ya Mvita, Changamwe, Kisauni,Jomvu na Likoni zikiathirika hii leo.
Katika hotuba ya kila siku katibu mkuu msimamizi katika wizara ya afya Dr. Rashid Aman amesema kuwa hakuja ripotiwa kisa chochote cha vifo kutokana na sampuli 1, 682 zilizopimwa jana , idadi ya vifo kisalia 577.
Hata hivyo watu wengine 318 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumba hivyo basi kuzidisha idadi ya waliopona hadi 20, 211. Kati yao 263 wamepona wakiwa katika uangalizi wa nyumbani na 55 wakitokea katika vituo mbali mbali vya afya nchini.