Pigo kwa wizara ya elimu korti ya juu ikipiga breki hatua za mwisho kuanzisha elimu mitaani na vijijini.
Mpango wa serikali ya Kenya wa kuanzisha masomo kwa wanafunzi wa shule za sekondari na za msingi katika maeneo wazi vijijini na mitaani almaarufu kama COMMUNITY- BASED LEARNING baada ya shule zote kufungwa kutokana na janga la Covid-19 imepata pigo baada ya Korti ya juu Jumanne 25 Agosti kuzia Wizara ya Elimu kuanzisha mpango huo.
Jaji James Makau alitoa agizo la muda kwa Waziri wa Elimu George Magoha kufuatia ombi la kundi la wazazi unaoongozwa na mzazi mmoja kwa jina Joseph Enock Aura, kupinga uamuzi wa serikali wa kufunga shule hadi sasa.
Bwana Aura anasema uamuzi wa kufunga shule ni ukiukaji wa haki za wanafunzi na ni kinyume na vifungu vya Sheria ya msingi kwa watoto.
Anataka korti iamue uhalali wa maagizo ya Rais Uhuru Kenyatta mnamo Machi 15 wa kufunga shule zote kufuatia athari za korona nchini.
Kulingana na Aura, maagizo hayo ni ya kutiliwa shaka kwani hayakuchapishwa kwenye Gazeti la Kenya au kutawazwa kwenye Bunge la Kitaifa kwa mjadala na idhini.
Bwana Aura anasema kufungwa kwa shule sio suluhisho la suala la afya ya umma
kufungwa kwa shule hadi tarehe kusikojulikana na ukiukaji mkubwa wa haki za watoto, sioni ithibati kuwa kufungwa kwa shule hadi mwaka ujao utasuluhisha changamoto zinazotukumba kwa sasa …,” inasoma ombi hilo.
Bwana Aura anataka mahakama ielekeze serikali kulipa fidia shule za msingi na sekondari kwa hasara zilizopatikana kutokana na kufungwa
Anataka mahakama kutoa maagizo ya kulazimisha wizara ya elimu kufungua tena taasisi za elimu kutoka Septemba 1. Kesi hiyo itatajwa mnamo Septemba 9.