Harambee stars kuchuana na Taifa Stars katika mechi ya kirafiki

Mchezaji wa Harambee Stars (kulia) akipewa usaidizi na mlinda lango wa Taifa Stars wakati wa mechi ya kirafiki
Mchezaji wa Harambee Stars (kulia) akipewa usaidizi na mlinda lango wa Taifa Stars wakati wa mechi ya kirafiki

Timu ya taifa Harambee Stars inatarajiwa kuwaalika majirani wao wa Tanzania, Taifa Stars katika Uwanja wa Nyayo jijini Niarobi katika mechi yao ya kirafiki.

Mechi hiyo itakayochezwa tarehe 29 mwezi Mei itakuwa ya kujipima nguvu kwenye mechi ya marudio na Congo itakayozaragazwa tarehe 4 mwezi juni jijini Nairobi.

Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini FKF,Robert Muthoni amesema kuwa wamewandaa vilivyo vijana hao wa nyumbani dhidi ya mechi yao na Congo.

Harambee Stars wanashikilia mkia katika kundi E wakiwa na alama moja pekee ,tayari wakiwa wametupwa nje katika michuano ya kufuzu kwa kombe la bara la Afrika Mwaka ujao.

Guinea Bissau wanashikilia nafasiĀ  ya kwanza katika kundi hilo wakiwa na alama 7 huku Zambia na Congo wakifuatia na alama 6 kila mmoja.