Nkaissery amuonya Joho

Waziri wa usalama wa kitaifa Joseph Nkaissery amemwonya gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho kuwa maafisa wa usalama wapo radhi kumkamata iwapo kufikia saa nane hii leo hatokuwa amerudisha bunduki anazomiliki.
Katika kikao na kamati ya bunge la Senate kuhusu masuala ya haki za kibinadamu Nkaissery ametofautiana na msimamo wa Joho akisema anaweza tu kukataa rufaa baada ya kurejesha bunduki hizo.
Amesema serikali pia ilikuwa inampokonya mbunge wa Kabete Ferdinard Waititu bunduki zake baada ya kuzuka makabiliano kati yake na Joho wakati wa uchaguzi mdogo wa Malindi akisema makabiliano kama hayo yalikuwa hatari.
Aidha Nkaissery ametetea kutumika kwa maafisa wa jeshi katika uchaguzi mdogo wa Malindi akisema walikuwa wakishika doria kutokana na matatizo ya kiusalama.