Wawakilishi wa wadi ya Nairobi wamtimua ofisini spika wao Beatrice Elachi
Kizazaa chatokea katika ofisi ya spika wa bunge wa kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi, baada ya kuregea ofisini mapema hii leo.
Elachi, ambaye alitimuliwa kutoka ofisi hiyo alielekea mahakamani kutaka kuregeshwa ofisini baada ya baadhi ya wakilishi wa wadi kumtuhumu kwa ufisadi na matumuzi mabaya ya ofisi .
Spika huyo akiwa na wafuasi wake katika ofisi hiyo, amesisitiza kuwa waliokuwa wanataka kumuondoa katika kiti cha bunge walikuwa na sababu ya kunyanyasa wengine ili wafaidike wao.