Viongozi wa Kiislamu wataka waathiriwa katika ghasia za uchaguzi mkuu uliopita wafidiwe

 

Viongozi wa Kiislamu wa vyama vya SUPKEM na CIPK Uasin gishu wameitaka serikali kuhakikisha waathiriwa waliosalia kufidiwa na serikali wametamubiliwa vilivyo na waweze kufidiwa kwa wakati ufao.

Wakiogozwa na sheikh Abubakar Bini viongozi hao wamesema kufanya hivyo kutaimarisha juhudi za maridhiano halisi miongoni mwa wakenya haswa baada ya kesi za ICC kutupiliwa mbali.

Kwa upande wake Sheikh Abdikadir Mohammad wa SUPKEM ameitaka serikali sasa kuwahudumia wakenya vilivyo baada ya kutupiliwa mbali kesi hizo huku wakitoa mwito wa kusamehewa na kurejeshwa nyumbani vijana walioshawishika kutoa ushahidi wa uwongo.