Margret Kenyatta nchini Marekani kupokea vifaa vya afya

Mama wa taifa,Magret Kenyatta amewasili mjini Phoeneix nchini Marekani kwa ziara ya siku 6 nchini humo ambapo atapokea vifaa vya afya vya kuendesha kampeni ya Beyond Zero.
Masuala mengine ambayo ameratibiwa bi Kenyata ni kukutana na washirika wake wa kampeni hiyo kabla ya kuhutubia wanafunzi a shule moja nchini humo.
Vifaa hivyo vinavyogharimu shilingi millioni 45 vinatarajiwa kupelekwa katika hospitali ya Chemolingot iliyoko Pokot mashariki katika kaunti ya Baringo, huku vifaa vyengine vikielekea katika hospitali zilizona uhaba wa vifaa nchini.