ICC kutoa uamuzi wa mlekeo wa kesi ya Ruto ya Sang

images (4)

Mahakama ya kimataifa ya ICC inatarajiwa kutoa uamuzi ambao utaashiria hatima ya naibu rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang’ kuhusu kesi inayowakabili katika mahakama hiyo.

Mahakama hiyo itatoa uamuzi wake iwapo itakubali kutumika kwa ushahidi uliokataliwa na mashahidi au itautupilia mbali na kuamua mwelekeo wa kesi ya wawili hao.

Ruto na Sang’ wameshatkiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kuhusiana na ghasia zilizotokea nchini baada ya uchaguzi mkuu wa 2007.

Mashtaka kama hayo yaliyomkabili rais Uhuru Kenyatta yalifutiliwa mbali na mwendesha mkuu wa mashataka ya ICC Fatou Bensouda kwa ukosefu wa ushahidi.

Ruto na Sang’ wameelezea imani ya kesi dhidi yao kutupiliwa mbali wakisema hawana hatia yeyote.